Migogoro
Watu wasiopungua 24 wameuwawa kwa shambulio la droni Sudan
8 Februari 2026
Matangazo
Kulingana na Shirika la Mtandao wa madaktari wa Sudan, shambulio hilo lilililenga gari lililokuwa limezibeba familia za watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao, kutokana na machafuko. Watu wengine kadhaa ambao idadi yao haijatajwa wamejeruhiwa na walipelekwa hospitali mjini Rahad.
RSF washutumiwa kuhusika na shambulio
Kundi la wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) linadaiwa kuhusika na shambulizi hilo, siku moja baada ya jingine lililoulenga msafara wa wahisani kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP. Wanamgambo hao wanaopambana na jeshi rasmi la Sudan, hawajatoa kauli yoyote kuhusiana na tukio hilo.