1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watano wafariki Ujerumani mkesha wa mwaka mpya 2025

1 Januari 2025

Watu watano wamefariki nchini Ujerumani huku afisa mmoja wa polisi amejeruhiwa vibaya kutokana na ajali zinazofungamana na matukio ya kurushwa kwa fashifashi za kusherehekea mwaka mpya.

Mkesha wa mwaka mpya I 2025 I Berlin
Afisa wa polisi akishika doria wakati wa sherehe za mkesha wa Mwaka Mpya karibu na Lango la Brandenburg mnamo Januari 01, 2022 mjini Berlin, Ujerumani.Picha: Adam Berry/Getty Images

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini humo.

Msemaji wa polisi Florian Nath amesema maafisa 13 wa polisi wamejeruhiwa, akiwemo mmoja aliyepata majeraha mabaya.

Spma pia: Dunia yaikaribisha 2025 baada ya mwaka wa olimpiki, misukosuko na Trump 

Watu 330 wamekamatwa katika mji mkuu Berlin usiku wa kuamkia leo huku taarifa ya polisi ikieleza kuwa, tofauti na miaka ya nyuma, mwaka huu mpya haukushuhudia matukio makubwa ya vurugu wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya.

Wajerumani husherehekea mwaka mpya kwa kurusha fashifashi, hali ambayo husababisha mijadala ya mara kwa mara juu ya kupiga marufuku fashifashi zinazoonekana kuwa hatari, hasa kutokana na idadi ya majeruhi kila mwaka, uchafuzi wa mazingira na kelele.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW