1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroChina

Watu watano wajeruhiwa China na guruneti kutoka Myanmar

4 Januari 2024

Chombo cha habari cha kitaifa cha China kimeripoti kwamba bomu la kurushwa kwa mkono lililokuwa limeelekezwa vibaya lilikipiga kijiji kidogo cha mji wa China wa Nansan kutokea Myanmar jana Jumatano.

Watu watano walijeruhiwa katika mlipuko uliotokea. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China  Wang Wenbin, amesema China tayari imewasilisha malalamiko rasmi ya kidiplomasia kwa pande husika kufuatia tukio hilo katika eneo la mkoa wa kusini mashariki wa Yunnan.

Hali katika eneo la Kokang kaskazini mwa Myanmar linalopakana na China imezorota katika wiki chache zilizopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW