1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yafanya mashambulizi ya anga Ukingo wa Magharibi

27 Agosti 2024

Watu watano wameuwawa kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi katika ardhi ya Wapalestina katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina.

 Ukingo wa Magharibi | Israel
Watu wakitathmini athari za shambulizi la Israel Ukingo wa MagharibiPicha: Jaafar Ashtiveh/AFP/Getty Images

Watu watano wameuwawa kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi katika ardhi ya Wapalestina katikamashambulizi ya angayaliyofanywa na Israel, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina. Israel imesema mashambulizi yake yalilenga kuharibu eneo linalotumiwa na wanamgambo Wakipalestina kuendesha harakati zao, katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams.

Shambulizi la Israel laua watano Ukingo wa Magharibi

Wakati huohuo Israel imetangaza amri mpya ya kuwataka Wapalestina katika mji wa Deir al Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza waondoke mara moja kabla ya kuanza operesheni nyingine ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas. Tangazo la Israel limetolewa wakati mazungumzo magumu ya kutafuta makubaliano ya kusitisha vita yakitarajiwa kuendelea mjini Cairo nchini Misri. Umoja wa Mataifa umelazimika kusitisha operesheni zake za kutowa msaada katika Ukanda wa Gaza kufuatia tangazo jipya la Israel katika mji wa Deir al Balah.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW