1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watano wameuwawa katika shambulizi Lamu

25 Juni 2023

Raia watano wameuwawa mapema leo, baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha katika vijiji viwili vya Salama na Juhudi vilivyo katika kaunti ya Lamu kusini mashariki mwa Kenya.

Somalia Mogadishu | Al-Shabaab Kämpfer während Militärübung
Picha: Farah Abdi Warsameh/AP/picture alliance

Taarifa ya jeshi la polisi nchini humo imesema washambuliaji hao pia walichoma nyumba na kufanya uharibifu wa mali katika tukio iliyoliita kuwa ni la kigaidi na baadaye walikimbilia msituni.

Soma pia: Ukuta kujengwa Lamu kuwazuia magaidi

Mmoja wa waliouwawa ni mwanamume mwenye miaka sitini ambaye alifungwa kamba na kisha kukatwa koo na nyumba yake ikateketezwa. Watu wengine wa tatu waliuwawa kwa namna hiyo hiyo huku mtu wa tano akiuwawa kwa kupigwa risasi.

Kaunti ya Lamu iko karibu na mpaka wa Kenya na Somalia na wapiganaji wa al Shabaab, wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara kama juhudi za kuishinikiza serikali ya Kenya iwaondoe wanajeshi wake Somalia.

Wanajeshi hao ni sehemu ya vikosi vya kulinda amani vya kimataifa vinavyoilinda serikali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW