1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Watu watano wauawa katika shambulio la Israel mjini Damascus

20 Januari 2024

Watu watano wamekufa kufuatia shambulio la makombora la Israel lililolenga jengo ambalo "viongozi wenye mafungamano na Iran" walikuwa wakikutana katika eneo la Mazzeh, magharibi mwa Damascus.

Shambulio la Israel mjini Damascus
Shambulio la Israel mjini DamascusPicha: Sana/REUTERS

Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria, lenye makao yake mjini London, Uingereza, limesema shambulio hilo lililenga jengo la ghorofa nne na kusababisha vifo vya watu watano.

Eneo la Mazzeh lina nyumba za wanadiplomasia kadhaa wakiwemo wa Lebanon na Iran.

Shambulio hilo linatokea katikati ya mzozo kati ya Israel na kundi la Hamas ambapo maelfu ya watu wameuawa katika ukanda wa Gaza.

Mwezi uliopita, shambulio la anga la Israel mjini Damascus lilimuua mshauri wa jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu wa Iran jenerali Seyed Razi.