1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu watano wauawa Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi

5 Oktoba 2025

Watu watano wameuawa nchini Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi usiku wa kuamkia Jumapili.

Lviv 2025 | Mashambulizi ya Urusi yalisababisha vifo vya watu 4
Maafisa wa vikosi vya zimamoto wakiwa kazini huko Lviv baada ya mashambulizi ya UrusiPicha: State Emergency Service of Ukraine in Lviv region/Handout via REUTERS

Wanne kati ya hao wameuawa katika jimbo la Lviv linalopakana na Poland ambayo ni mwanachama wa NATO. Serikali ya Poland imesema imetuma ndege za kivita mapema leo katika eneo hilo la mpakani ili kuhakikisha usalama wa anga lake.

Rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky  amesema Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya makombora zaidi ya 50 na droni karibu 500. Maelfu ya watu wamesalia bila umeme katika jimbo la kusini mashariki la Zaporizhzhia ambako kumeripotiwa pia kifo cha mtu mmoja.

Urusi haijazungumzia chochote kuhusu shambulio hilo lakini katika siku za hivi karibuni, imezidisha mashambulizi yake na kuilenga miundombinu ya nishati ya Ukraine hasa wakati huu msimu wa baridi ukikaribia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW