1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Watu watatu wateketezwa moto DRC

26 Desemba 2023

Wanamgambo wa kundi lenye itikadi kali la ADF wanadaiwa kuwaua kwa kuwatekeza moto bibi na wajukuu zake wawili katika kijiji cha Kamwenge, magharibi mwa Uganda.

Kongo | Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC
Wanajeshi wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waendesha operesheni ya pamoja katika eneo la Beni.Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Kwa mujibu wa maafisa wa eneo hilo tukio hilo limetokea wiki moja baada ya watu wengine 10 kuuwawa katika eneo hilo na wanamgambo waADF.

Jeshi na polisi wa Uganda wanaendelea kuwasaka washambuliaji. Kundi la ADF linatuhumiwa kwa mauaji ya maelfu ya raia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika miaka ya hivi karibuni na pia kwa kufanya mashambulizi katika mpaka wa Uganda.

Soma pia: Jeshi la Uganda latangaza donge nono kuwanasa ADF

Uganda na Kongo zilianzisha operesheni za pamoja za kijeshi za kupambana na wanamgambo wa ADF mnamo Novemba 2021 lakini mashambulizi ya waasi bado yanaendelea.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW