1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watatu wauawa katika shambulizi la Israel, Gaza

10 Februari 2026

Mashambulizi ya kijeshi yaliofanywa na Israel jana Jumatatu yamewauwa watu watatu magharibi mwa mji wa Gaza. Haya ni kulingana na hospitali iliyowapokea majeruhi wa tukio hilo.

Maafisa wa uokoaji wabeba mwili wa muathiriwa wa shambulizi la Israel dhidi ya kituo cha polisi cha Sheikh Radwan, Gaza City
Shambulizi la Israel Gaza City mnamo Januari 31, 2026Picha: Omar Al-qattaa/AFP

Mashuhuda wa shambulizi hilo la Israel Gaza City, wanasema lililenga eneo la makazi na kusababisha vifo pamoja na majeruhi.

Wafanyakazi wa misaada ya dharura waliwasafirisha majeruhi kwa ambulensi huku wakazi wakibeba mwili kuelekea chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Shifa.

Mmoja wa mashuhuda hao amesema jengo lililolengwa linaishi watoto peke yake na akatilia mashaka uwezekano wa kupatikana kwa amani huku akielezea kughadhabishwa na Israel pamoja na Marekani.

Hospitali ya Shifa iliripoti vifo hivyo kati kati mwa kipindi cha mwezi mmoja wa kusitisha mapigano ambacho bado mapigano yamekuwa yakiendelea.

Hapo jana, jeshi la   Israel lilisema kuwa linalenga shabaha zake kwa kujibu mashambulizi dhidi ya vikosi vyake katika mji wa kusini wa Rafah ambao linasema ni ukiukwaji wa makubaliano hayo ya kusitisha mapigano.

Suluhisho la mataifa mawili linawezekana?

13:10

This browser does not support the video element.

Guterres ana wasiwasi kuhusu uamuzi wa Israel

Kwa upande wake, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi kuhusu uamuzi wa baraza la usalama la la kuimarisha udhibiti wa nchi hiyo katika eneo lililokaliwa la Ukingo wa Magharibi.

Katika taarifa iliyosomwa na msemaji wake Stéphane Dujarric, ameonya kuwa uamuzi huo wa Israel unaweza kusambaratisha uwezekano wa suluhisho la mataifa mawili.

Ameongeza kuwa hatua kama hizo zinazojumuisha uwepo wa Israel katika Ukanda wa Gaza sio kwamba tu zinadhoofisha usalama lakini pia kinyume cha sheria kama ilivyotajwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ.

Ziara ya Netanyahu nchini Marekani, inakuja wiki mbili tu baada ya mjumbe maalumu wa Rais wa Marekani Donald Trump, Steve Witkoff na mshauri wa masuala ya Mashariki ya Kati Jared Kushner kukutana na Netanyahu mjini Jerusalem.

Kulingana na ofisi ya Netanyahu, waziri huyo mkuu anaamini kwamba mazungumzo yoyote lazima yajumuishe makombora ya masafa marefu na kukomesha msaada kwa makundi ya wanamgambo yanayoungwa mkono na Iran kama vile Hamas na Hezbollah nchini Lebanon.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu atakutana na Trump wiki mbili baada ya ujumbe wa Marekani kufanya ziara nchini Israel.Picha: Abir Sultan/AP Photo/picture alliance

Ufanisi mdogo katika mazungumzo ya nyuklia

Miaka kadhaa ya mazungumzo ya nyuklia yamepata ufanisi mdogo tangu Trump alipofutilia mbali makubaliano ya mwaka 2015 na Iran, kwa kuungwa mkono na

Iran imeonyesha nia ndogo ya kushughulikia masuala mengine, hata baada ya kukumbwa na vikwazo vya mara kwa mara.

Lakini mkutano na Trump unampaNetanyahu fursa ya kuongoza mchakato huo na pia kunaweza kuimarisha uungwaji mkono nyumbani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW