1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAustralia

Watu watatu wauawa kwa risasi New South Wales, Australia

22 Januari 2026

Polisi nchini Australia wameanzisha msako baada ya tukio la mauaji lililotokea katika jimbo la New South Wales ambapo watu watatu wameuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya.

Australia Sydney 2026 | Maafisa wa polisi | Ufukwe wa Bondi
Polisi wa Australia wakishika doria katika ufukwe wa BondiPicha: George Chan/Getty Images

Tukio hilo limezua taharuki katika mji mdogo wa Lake Cargelligo, ulioko takriban kilomita 611 magharibi mwa Sydney, huku wakazi wakihimizwa wabaki majumbani kwa ajili ya usalama wao.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, wanawake wawili na mwanamume mmoja wameuawa katika tukio hilo la jioni, huku mwanamume mwingine akipelekwa hospitalini akiwa katika hali mbaya lakini thabiti.

Gazeti la Sydney Morning Herald limeripoti kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kujificha ndani ya mji huo akiwa na silaha.

Polisi wameweka vizuizi katika maeneo kadhaa na kuwataka wananchi kuepuka maeneo ya tukio na kutoa taarifa yoyote watakayokuwa nayo kuhusu mshukiwa huyo.

Shambulio hilo la risasi limetokea wiki chache tu tangu tukio jingine baya la risasi kutokea kwenye ufukwe wa Bondi wakati wa hafla ya Hanukkah, ambapo watu 15 waliuawa. Tukio hilo lilitajwa kuwa shambulio baya zaidi la risasi nchini Australia katika kipindi cha miongo kadhaa, na liliibua mjadala kuhusu usalama wa umma na udhibiti wa silaha.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW