1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 3 wauwawa katika shambulio chuo kikuu cha Michigan

14 Februari 2023

Polisi katika jimbo la Michigan nchini Marekani imesema, mshukiwa anaedaiwa kuwauwa watu watatu na kuwajeruhi watu wengine watano katika chuo kikuu cha Michigan jana usiku amejiua.

USA Ehemann Nancy Pelosis attackiert Anklage | Bill Scott
Picha: Justin Sullivan/Getty Images

Tangazo hilo limetolewa mapema leo asubuhi masaa manne baada ya tukio hilo kuripotiwa.

Mshukiwa huyo wa kiume aliye na miaka 43hana mafungamano yoyote yanayojulikana katika chuo kikuu hicho, wala nia ya mashambulizi yake haijajulikana.

Soma pia:Marekani yauwa wapiganaji wasiopungua 12 wa Al-Shabaab Somalia

Watu waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali moja katika jimbo hilo na wameripotiwa kuwa katika hali mbaya.

Taarifa zaidi juu ya tukio hilo hazijatolewa lakini Naibu Mkuu wa Polisi kwenye chuo hicho, Chris Rozman, amesema ufyatuaji risasi ulisikika katika maeneo mawili ya chuo hicho. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW