1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asili na mazingiraAfrika Kusini

Watu wawili wafariki dunia baada ya kukwama kwenye theluji

23 Septemba 2024

Watu wawili wamefariki dunia baada ya kukwama kwenye theluji iliyosababishwa na baridi kali katika jimbo la kwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.

Theluji yasababisha vifo
Picha ya theluji juu ya msitu wa mlima. Watu wawili wamekufa kwa kukwama kwenye theluji iliyosababishwa na baridi kali katika jimbo la kwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.Picha: Angelika Warmuth/REUTERS

Jeshi la ulinzi limepelekwa ili kusaidia zoezi la uokoaji, ikiwemo kusafisha barabara na kuondoa theluji nzito zilizoganda juu ya nyumba jimboni humo.

Mamlaka ya hali ya hewa imewaonya wakazi wa KwaZulu-Natal, kusalia majumbani kwa siku chache zijazo, kwani hali mbaya ya hewa inatarajiwa kuendelea katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo.

Wakati huo huo Chama cha Wapigania Uhuru wa Kiuchumi EFF, kimeilaumu serikali kwa kuchelewa kutoa msaada kwa watu waliokwama na kinataka huduma za dharura ikiwemo magari ya kusafisha barabara na matibabu vinatolewa, ili kuzuia maafa zaidi.

Siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, idadi kubwa ya madereva na wasafiri walikwama kwenye barabara kuu inayounganisha jiji la Johannesburg na Durban, baada ya kuzuiwa na theluji kubwa iliyonyesha.