1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wawili wafariki Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi

21 Septemba 2023

Miji kadhaa ya Ukraine imelengwa usiku wa kuamkia leo na mashambulizi makubwa ya Urusi na kusababisha vifo vya watu wawili huko Kherson. Watu kadhaa katika mji mkuu wa Kyiv wamejeruhiwa.

Ukraine Russischer Drohnenangriff über Kiew
Picha: Roman Petushkov/Xinhua/picture alliance

Mamlaka za Ukraine zisema mashambulizi hayo yameharibu miundombinu ya nishati na kusababisha kukatika kwa umeme.

Zelensky atoa mwito wa kupatiwa silaha zenye nguvu zaidi

Mashambulizi hayo yanajiri wakati Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine  akifanya ziara yake ya pili nchini Marekani katika jitihada za kupata msaada zaidi wa kupambana na wavamizi wa Urusi licha ya dalili kuonyesha kwamba miongoni mwa wabunge wa Marekani wamechoshwa na mzozo huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW