1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 2 wauawa kwa kufyatuliwa risasi huko Hamburg, Ujerumani

26 Machi 2023

Polisi nchini Ujerumani imefahamisha leo kuwa watu wawili wamekufa baada ya shambulio la risasi huko Hamburg.

Deutschland | Zwei Tote nach Schüssen in Hamburg
Picha: Jonas Walzberg/dpa/picture alliance

Hili ni tukio la pili mnamo mwezi huu katika mji huo wa bandari unaopatikana Kaskazini mwa Ujerumani.

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma imebaini kuwa waliouawa ni wanaume wawili na mmoja wao ni mshukiwa wa tukio hilo ambaye inasadikika kuwa baada ya kumuua mtu mmoja alijiua.

Soma pia: Waliouwawa kwa risasi Hamburg wafikia 8

Jarida la Bild liliripoti kwamba hapo jana polisi waliitwa muda mfupi kabla ya saa sita usiku na kwamba magari 28 yaliwasili eneo la tukio. Polisi wamesema walikuwa wamehitimisha operesheni hiyo na sasa wanaendelea na uchunguzi. Msemaji wa polisi hakutoa maelezo zaidi juu ya mhalifu wa tukio hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW