1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Watu 2 wauliwa nje ya ubalozi wa Marekani Jeddah

Josephat Charo
29 Juni 2023

Watu wawili wameuliwa kwenye makabiliano ya risasi nje ya ubalozi wa Marekani katika mji wa bandari wa Jeddah nchini Saudi Arabia.

Indonesien, Jakarta | Fussweg vor US-Botschaft nach 21 Jahren wieder zugänglich
Picha: Pradita Utama/detikcom

Taarifa hiyo imeripotiwa hivi leo na shirika la habari la serikali la Saudia SPA. Shirika hilo limemnukuu afisa wa polisi akisema mwanamume mmoja aliyekuwa amejihami kwa bunduki ameuwawa wakati wa makabiliano ya risasi na maafisa wa usalama jana Jumatano karibu na ubalozi huo wa Marekani.

Msemaji wa jeshi la polisi ukanda wa Mecca amesema mtu aliyekuwa akiendesha gari dogo alisimama karibu na jengo la ubalozi na kutoka nje akiwa amebeba silaha mkononi, maafisa wa usalama wakamkabili na ufyetulianaji wa risasi ukasababisha kifo chake.

Pia amesema mlinzi raia wa Nepal alijeruniwa na baadaye kufariki. Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimesema hakuna raia wa Marekani aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW