1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wawili wauwawa kufuatia shambulizi la Urusi Kharkiv

Josephat Charo
13 Januari 2026

Watu wawili wameuliwa katika shambulizi la Urusi lililofanywa katika mji wa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine.

Watu wawili wameuwawa katika shambulizi la Urusi mjini Kharkiv nchini Ukraine
Watu wawili wameuwawa katika shambulizi la Urusi mjini Kharkiv nchini UkrainePicha: Stringer/Anadolu/picture alliance

Shambulio la Urusi katika mji wa Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine limewaua watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Taarifa hiyo imetolewa mapema leo na gavana wa mkoa Oleg Synegubov akisema kufikia sasa, watu wawili wanajulikana kuuawa na mashambulizi ya adui nje kidogo ya Kharkiv,  akiandika kwenye mtandao wa Telegram.

Pia alisema watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulio hilo la usiku kucha.

Urusi imeishambulia Ukraine kwa ndege zisizo na rubani na makombora ya kila siku katika miezi ya hivi karibuni, ikilenga miundombinu ya nishati na kukatisha umeme katika kilele cha baridi kali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW