JamiiAsia
Watu wengine 44 waokolewa tetemeko la Taiwan
4 Aprili 2024Matangazo
Hayo ni kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Taiwan, Lin You-chang, jioni ya Alkhamis (Aprili 4).
Katika ripoti ya shirika la habari la serikali (CNA), Waziri Lin You-chang alisema watu hao walikuwa wamenasa kwenye njia mbili za chini ya ardhi.
Soma zaidi: Takribani watu 1,000 wajeruhiwa katika tetemeko la ardhi Taiwan
Ripoti hiyo pia ilisema maafisa waliwaokoa watu wengine tisa waliokuwa kwenye pango.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Taiwan, kufikia sasa maafisa wamewaokoa watu takriban 70 na kuwapeleka katika maeneo salama kufuatia tetemeko hilo la ardhi.
Maafisa bado hawajapata mawasiliano na watu wengine watatu kutoka Canada na Australia, ambao hawajulikani walipo.