1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wengine 6 wauwawa kwenye maandamano ya upinzani Senegal

3 Juni 2023

Serikali ya Senegal imesema watu wengine sita wameuwawa jana Ijumaa baada ya mapambano kati ya polisi na waandamanaji wanaounga mkono upinzani.

Senegal Unruhen nach Urteil gegen Sonko
Picha: Guy Peterson/AFP

Idadi hiyo mpya ya vifo, inafanya jumla ya watu waliouwawa baada ya maandamano yaliyoanza Alhamisi kufikia watu 15.

Soma zaidi: UN na AU zahimiza amani kufuatia machafuko Senegal

Kulingana na taarifa ya msemaji wa serikali, Maham Ka, vifo vinne kati ya vilivyoripotiwa Ijumaa, vilitokea katika eneo la Dakar na viwili vilitokea Ziguinchor. 

Vurugu zilizuka Alhamisi baada ya mpinzani mkubwa wa Rais Macky Sall, Ousmane Sonko  kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kuwachochea vijana.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW