1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Watu wenye silaha waua askari 23 Syria

11 Agosti 2023

Watu wenye silaha wamelishambulia basi lililowabeba wanajeshi wa Syria na kuwaua takribani askari 23.

Bendera inayotumiwa na Kundi linalojiita Dola la Kiislamu
Kundi linalojiita Dola la Kiislamu limekuwa likifanya hujuma nchini Syria karibu muongo mmoja uliopitaPicha: CPA Media/picture alliance

Shirika linalofuatilia haki za binaadamu nchini Syria, limesema shambulizi hilo limetokea mapema leo asubuhi, ambapo wanajeshi wengine 10 wamejeruhiwa.

Inadaiwa kuwa shambulizi hilo limefanywa na wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

Kwa mujibu wa shirika hilo lenye makao yake mjini London, Uingereza, wanamgambo wamelishambulia basi hilo katika mkoa wa Deir al-Zour, mashariki mwa Syria.

Hata hivyo, hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa na IS wala serikali kuhusu mauaji hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW