Watu wenye silaha wamewaua takribani watu 56 Nigeria
20 Aprili 2025
Matangazo
Mapigano kati ya wafugaji wa kuhamahama na wakulima kuhusu matumizi ya ardhi ni ya kawaida katikati mwa Nigeria. Awali gavana wa eneo hilo Hyacinth Alia alionesha kuwanyooshea kidole jamii ya wafugaji kuhusika na vurugu za maeneo ya Ukum na Logo. Kwa vile wafugaji wengi watoka katika jamii ya Kiislamu ya kabila laFulani,na wakulima wengi katika uumini wa Kikristo mashambulizi katika eneo linaloitwa Middle Belt mara nyingi huchukua mwelekeo wa kidini au kikabila.