1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Watu zaidi 2,000 wafa kwa tetemeko la ardhi Afghanistan

9 Oktoba 2023

Watu zaidi ya 2,000 wamekufa kutokana na tetemeko la ardhi nchini Afhgahisntan, huku utawala wa nchi hiyo umesema matetemeko kadhaa yaliikumba magharibi mwa nchi mwishoni mwa wiki.

Watu wakiendelea kutafuta waathirika waliokwama kwenye maporomoko baada ya tetemeko Afganistan
Watu wakiendelea kutafuta waathirika waliokwama kwenye maporomoko baada ya tetemeko AfganistanPicha: Gulrahim Niazman/AP/picture alliance

Mitetemeko hiyo ilisikika pia katika nchi jirani ya Iran. Kwa mujibu wa taarifa zaidi, watu wengine wapatao 9,240 wamejeruhiwa.

Shirika la Jiolojia la Marekani limesema mojawapo ya matetemeko lilifikia kipimo cha 6.3 kwenye mji wa Herat magharibi mwa Afghanistan.

Soma pia:Tetemeko la ukubwa wa 6.3 lapiga Magharibi mwa Afganistan

Maafisa wa uokoaji wanaendelea kuwatafuta watu walionusurika na miili ya wahanga wa tetemeko hilo.

Mataifa jirani, Pakistan na Iran, yamesema yatawapeleka pia maafisa wa uokoaji nchini Afghanistan.