1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Watu zaidi 30 wauwawa katika shambulio la kujitoa muhanga

30 Januari 2023

Zaidi ya watu 30 wameuwawa leo baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujiripua ndani ya msikiti mmoja uliofurika waumini kwenye mji wa kaskazini magharibi mwa Pakistan wa Peshawar.

Pakistan | Explosion in einer Moschee in Peshawar
Picha: MAAZ ALI/AFP/Getty Images

 Duru za maafisa wa serikali zinasema watu wengine 150 wamejeruhiwa na kuna wasiwasi idadi ya vifo huenda itaongezeka.

Wengi ya waliouwawa ni maafisa wa polisi na inaarifiwa kulikua na takribani waumini 350 wakati mshambuliajihuyo alipojiripua.

Soma pia:Pakistan: Mshambuliaji wa kujitoa muhanga awaua watu zaidi ya 30 waliokuwa msikitini

Kamanda wa kundi la Taliban nchini Pakistan amedai kuhusikana mpango wa shambulizi ambalo limelaaniwa vikali na viongozi wa serikali na upinzani nchini Pakistan.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW