Ajali ya boti yauwa zaidi ya watu 10 DRC
14 Februari 2024Matangazo
Akielezea tukio hilo mmoja kati ya maafisa wa serikali katika eneo hilo, Eliezer Ntambwe amesema boti hizo mbili ambazo zilikuwa na idadi kubwa ya mizigo na abiria ziligongana Jumatatu katika eneo la mto huo huko mashariki mwa mji mkuu, Kinshasa. Hata hivyo haijaweza pia kufahamika idadi gani ya watu imefanikiwa kuokolewa katika ajali hiyo.Vyombo vya usafiri nchini Kongo vinamilikiwa na watu binafsi, na maafisa wamekuwa wakionya kuwa hawafuati masharti ya usalama wa wasafiri. Januari ilitokea ajali ya boti ambapo watu 50 walitangazwa kupoteza maisha.