1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaIraq

Karibu watu 100 wafariki katika kisa cha moto nchini Iraq

27 Septemba 2023

Karibu watu 100 wamekufa na wengine 150 wamejeruhiwa baada ya moto kuzuka kwenye sherehe ya ndoa katika wilaya ya Hamdaniya, jimbo la Nineveh nchini Iraq.

Vikosi vya uokozi vikiwa nje ya hospitali ya Hamdaniyah ambako majeruhi wa ajali ya moto kwenye harusi nchini Iraq Septemba 27, 2023 walipelekwa
Vikosi vya uokozi vikiwa nje ya hospitali ya Hamdaniyah ambako majeruhi wa ajali ya moto kwenye harusi nchini Iraq Septemba 27, 2023 walipelekwaPicha: ZAID AL-OBEIDI/AFP/Getty Images

Vyombo vya habari vya Iraq vimesema idara za ulinzi kwenye eneo hilo zimesema moto huo uliwaka katika ukumbi huo ambako hufanyika shughuli kubwa, baada ya kurushwa fataki wakati shughuli hiyo ikiendelea. 

Kulingana na vyombo hivyo vya habari, idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Taarifa za awali zimesema jengo hilo limejengwa kwa vifaa vya ujenzi vinavyoshika moto kwa haraka, na kusababisha jengo kuanguka muda mfupi baada ya kushika moto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW