1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu zaidi ya 20 wauawa katika mashambulio ya Istanbul

16 Novemba 2003

ISTANBUL: Nchini Uturuki waliuawa si chini ya watu 20 yaliposhambuliwa mahekalu mawili ya Kiyahudi mjini Istanbul, kwa mujibu wa tarakimu rasmi. Watu zaidi ya 300 walijeruhiwa katika miripuko hiyo miwili ya magari. Baadhi ya majuruhi wanaendelea kutapia maisha yao. Taasisi za usalama za Kituruki zinashutumu kwamba mashambulio yote mawili yamefanywa na kundi la kigaidi, alisema Waziri wa Mambo ya Ndani Abdulkadir Aksu. Mashambulio hayo mawili yalifanyika karibu wakati mmoja mbele ya Hekalu Kuu ya Neve-Shalom mtaani Beyoglu na karibu ya hekalu ya Sisli. Pia yaliteketezwa majengo kadha karibu ya vituo vya mashambulio hayo. Kwa kulingana na taarifa za serikali ya Israel, kadiri nusu ya watu waliouawa walikuwa Wayahudi. Hii leo Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel anatazamiwa kwenda Istanbul.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW