Migogoro
Zaidi ya watu 300 watekwa nyara Nigeria
7 Machi 2026
Matangazo
Mamlaka zimesema huenda shambulio hilo ni la kulipiza kisasi kutokana na operesheni ya jeshi iliyowauwa makamanda watatu wa kundi la Boko Haram. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na tukio hilo.
Mashambulizi mengine yazuiwa na polisi
Msemaji wa jeshi Uba Sani, amesema wanajeshi walifanikiwa kuyazuia mashambulizi mengine ya aina hiyo yaliyoshuhudiwa katika jamii za Konduga, Marte, Jakana, na Mainok kati ya Jumatano na Ijumaa wiki hii.
Nigeria inakabiliwa na kitisho cha usalama kutokana na makundi kadhaa ya wanamgambo wenye itikadi kali yakiwemo Boko Haram, ISWAP, Lakurawa na mengine yenye makao yake katika Ukanda wa Sahel.