1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu zaidi ya 6,000 wapoteza maisha kujaribu kuingia Ulaya

9 Januari 2024

Idadi hiyo ni takriban mara tatu zaidi ya iliyorikodiwa katika mwaka uliotangulia 2022, ambapo wahamiaji 2,390 walipoteza maisha.

Wahamiaji  wasiopungua 6,618 wapoteza maisha au kutoweka wakijaribu kuingia Ulaya kupitia baharini mwaka 2023
Wahamiaji wasiopungua 6,618 wapoteza maisha au kutoweka wakijaribu kuingia Ulaya kupitia baharini mwaka 2023Picha: Jeremias Gonzalez/AP/picture alliance

Shirika la kutetea haki za wahamiaji nchini Uhipania limesema wahamiaji wasiopunguwa 6,618 walikufa au kutoweka wakijaribu kuingia Uhispania kupitia njia ya bahari mwaka 2023.

Idadi hiyo ni takriban mara tatu zaidi ya iliyorikodiwa katika mwaka uliotangulia 2022, ambapo wahamiaji 2,390 walipoteza maisha.

Jumla ya watoto 384 ni miongoni mwa wahanga kwa mujibu wa shirika hilo linalokusanya data  kutoka kwa familia za wahamiaji waliokufa au kutoweka pamoja na takwimu  zinazotolewa na maafisa wa shughuli za uokoaji.

Vifo vingi vya idadi ya wahamiaji iliyotajwa vimetokea katika bahari ya Atlantiki, ambayo inatumiwa kama njia ya kutoka Afrika kuingia visiwa vya Canary vya Uhispania.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW