1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu zaidi ya 700,000 wakimbia machafuko Haiti

2 Oktoba 2024

Umoja wa Mataifa unasema kwamba zaidi ya watu 700,000 wameyakimbia makazi yao nchin Haiti, nusu yao wakiwa ni watoto, kutokana na kuongezeka kwa machafuko ya magenge ya uhalifu.

Haiti polisi magenge
Askari polisi wa Haiti akiwa nje ya gereza moja kukabiliana na magenge ya uhalifu.Picha: REGINALD LOUISSAINT JR/AFP/Getty Images

Shirika la Wahamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) lilisema hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba kwamba karibu watu 702,973 walikuwa wameondoka makwao.

Soma zaidi: Umoja wa Mataifa waongeza muda wa kikosi cha polisi Haiti

Kulingana na IOM, takwimu hizi mpya ni ongezeko la asilimia 22 ya idadi ya wakimbizi wa ndani tangu mwezi Juni, hali inayoashiria kuwa mzozo wa kiutu.

Shirika hilo limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuuchukulia kwa uzito zaidi mgogoro huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW