Washukiwa wawili wa ugaidi wauwawa Paris
18 Novemba 2015Kwa mujibu wa taratibu za jeshi la polisi afisa aliyetoa taarifa hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lakini aliongeza kusema mapambano yanaenendelea baada ya kudumu kwa takribani masaa matano. Mpaka wakati huu mtuhumiwa aliyejificha hajaweza kutambulika. Serikali inasema operesheni hiyo inalenga kumtia nguvuni mtu aliyepanga njama ya shambilizi la Ijumaa iliyopita mjini Paris ambapo takribani watu 129 waliuwawa.
Taarifa ya ofisi ya mwendesha mashitaka
Katika hatua nyingine ofisi ya mwendesha mashitaka imethibitisha kuwa mwanamke aliyejifunga viripuzi alijiripua wakati wa makabiliano kati ya polisi na watuhumiwa baada ya katika mashambilizi ya juma lililopita. Taarifa zinasema ni mmoja, miongoni mwa watu wawili waliouwawa katika operesheni inayoendelea katika viunga vya jiji la Paris vya Saint-Denis.
Wakati huo huo, katika kitongoji hicho cha Saint-Denis polsi imewza kuwaokoa wakazi 20, katika jengo ambalo watuhumiwa wa ugaidi, wenye kuhusishwa na mauwaji ya juma lililopita wamejifisha huku kukiwa na msuguano mkali na polisi.
Mtu aliyteambuliwa kwa jina moja la Ahmed anaishi jirani ya eneo la tukia alikuwa na haya "Tulikuwa tumelala, tumesikia sauti ya mlio wa risasi kutoka kwa polisi na mabomu kwa wakati mmoja. Kwa mara ya kwanza polisi hawakutruhusu tuondoke katika ghorofa, tulikwama ndani, hatkuweza kufungua mlango, hatukuweza kutazama nje kupitia madirishani, na kulikuwa na majibizano ya risasi kati ya polisi na magaidi".
Mwanamke mwengine jirani alitambuliwa kwa jina moja la Sabine pasipo jina la kwanza alikuwa haya "Ilikuwa jengo la juu. Polisi walivunja mlango na kutuzuia sisi tusitoke, walituamulu tulale chini, tusisogee, tuzime taa zote na hivyo ndivyo nilivyofanya. Nilijaribu kwenda chooni lakini kulikuwa miripuko na sikusikia kama dari linataka kuporomoka, kwa hivyo nikatoka kutafuta usalama kati ya mlango wa choo na chumba cha kulala na tukasalia kuwa hivi na mtoto wangu, tumeweza kuona risasi zikifyatuliwa, tumekuwa tuhisi jengo likitikisika"
Afisa mmoja wa jiji aliliambia shirika la habari AP kwamba wakati hao wamepeleka katika eneo lingine la ukimbi wa jiji kwa sababu za kiusalama. Jengo hilo la jiji lipo umbali wa mita 200 kutoka katika eneo ambalo, polisi inaendelea na operesheni zake.
Ujerumani kufanya mkutano maalamu wa usalama
Nje Ufaransa, nchini Ujerumani , Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na mawaziri waandamizi watafanya mkutano maalumu juu ya masuala ya kiusalama baada ya mchuano wa kandanda wa kimataifa kuahirishwa hapo jana jioni kutokana na hofu ya kuwepo kwa mpango wa kufanyika shambulizi. Jana usiku kutokana na kitisho cha bomu, mechi ya kandanda mjini Hannover kati ya Ujerumani na Uholanzi ilifutwa wakati mashabiki wakiwa njiani kuelekea uwanjani.
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka serikalini, mazungumzo hayo ambayo yatawahusisha maafisa wakuu katika Idara ya Usalama wa Taifa, utafanyika baada ya mkutano wa baraza la mawaziri. Makamo wa Kansela Sigmer Gabriel amesitisha majukumu yake kadhaa ili aweze kuhudhuria mkutano huo.
Kwengineko nchini Syria. katika kipindi cha masaa 72 makombora ya angani ya ndege za kijeshi za Urusi na Syria yameuwa kiasi ya wenye itikadi kali 33. Kwa mujibu wa taarifa za makundi ya waangalizi nchini humo idadi nyingine kubwa ya wanamgabo hao wamejeruhiwa katika mashambalizi hayo ambayo yalukuwa yakilenga maghala ya kuhifadhia silaha, kambi za jeshi na vituo vya ukaguzi.
Mkurugenzi wa shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu lenye makazi yake mjini London nchini Uningereza Rami Abdel Rahman ambae anategeme taarifa zake kutoka kwa watoa tiba, wanaharakati na vyanzo vingine nchini Syria amesema idadi kubwa ya wanamgambo wa Dola la Kiislamu waliouwawa walikuwa katika vituo vya ukaguzi.
Mwandishi: Sudi Mnette AP/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman