1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Watumishi 2 wa shirika la misaada ya Marekani wauawa, Amhara

11 Aprili 2023

Shirika la misaada la Kanisa katoliki la CRS limesema watumishi wake wawili wameuawa kwa kupigwa risasi mwishoni mwa wiki iliyopita katika jimbo la Amhara, kaskazini mwa Ethiopia, kulikoshuhudiwa maandamano hivi karibuni

Äthiopien Bahir Dar | Friedlicher Protest gegen Premierminister Abiy
Picha: Alemenew Mekonnen/DW

Tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili, kulipofanyika maandamano katika miji kadhaa ya Amhara ya kupinga mipango ya serikali ya kuvunja vikosi vya kikanda.

Shirika hilo la Marekani limesema waliouawa ni meneja wa usalama Chuol Tongyik na dereva Amare Kindeya, waliokuwa kwenye gari wakirejea Addis Ababa kutoka kwenye majukumu jimboni humo.

Mwakilishi wa CRS nchini humo, Zemede Zewdie amesema wanahuzunishwa sana na tukio hilo pamoja na machafuko yasiyo na maana, ingawa limeahidi kuendelea kuwasaidia watu wa Ethiopia.

 

 

    

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW