Waturuki waunga mkono mageuzi ya katiba
13 Septemba 2010Kuambatana na Waziri Mkuu Reccep Tayyip Erdogan, matokeo ya mwanzo ya kura hiyo ya maoni, yanaonyesha kuwa mpango huo umeungwa mkono kwa asilimia 58 baada ya asilimia 77 ya Waturuki kujitokeza kupiga kura zao.
Miongoni mwa mageuzi yatakayofanywa, haki za wananchi na udhibiti wa kiraia jeshini utaimarishwa.Kwa mujibu wa Erdogan, mabadiliko hayo ni hatua muhimu kwa Uturuki inayotaka kuingia katika Umoja wa Ulaya. Lakini viongozi wa upinzani wanamtuhumu Erdogan kuwa chama chake cha AKP kinataka kuwa na ushawishi zaidi katika mfumo wa sheria.
Wakati huo huo, mjini Berlin,waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema matokeo ya kura hiyo ya maoni ni hatua muhimu kwa Uturuki kuelekea Ulaya. Hata hivyo,mchakato wa mageuzi unapaswa kushughulikiwa zaidi.