1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watzke aamini mashabiki watarejea viwanjani

Josephat Charo
18 Mei 2021

Mkurugenzi Mkuu wa timu ya Borussia Dortmund amesema (18.05.2021) ana matumaini mashabiki wataruhusiwa kuingia viwanjani kutazama mechi za Bundesliga msimu ujao

Dortmund - Explosionen an BVB-Bus - Hans-Joachim Watzke
Picha: Getty Images/Bongarts/D. Mouhtaropoulos

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke anaamini mashabiki watarejea viwanjani msimu ujao lakini amekiiri bado kuna shaka ikiwa viwanja vitajaa kutokana na janga la virusi vya corona.

"Bila shaka nategemea mashabiki watakuwa viwanjani msimu ujao," aliliambia shirika la habari la Funke siku ya Jumanne.

"Swali lililopo tu ni idadi gani ya mashabiki wanaotakiwa kuruhusiwa. Asilimia thelathini ya watu wameshadungwa chanjo mara moja, watapata chanjo ya pili kufikia wakati huo. Haiwezekani kuwanyima kila kitu watu hawa. Wanatakiwa waruhusiwe wafurahie maisha ya kawaida tena."

Union Berlin wameruhusiwa kuwa na mashabiki 2,000 katika mechi yao ya mwisho ya msimu huu wa Bundesliga nyumbani watakapoumana na RB Leipzig Jumamosi kutokana na kupungua kwa maambukizi ya virusi vya corona katika mji mkuu Berlin.

Lakini miji mingine, ukiwemo Dortmund, haijafikia kiwango cha kuwaruhusu mashabiki kwenda kutazama mechi viwanjani.

(dpa)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW