1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Waumini 163 watekwa nyara kanishani Nigeria

20 Januari 2026

Makundi yenye silaha yamewateka nyara waumini 163 wa Kikristo baada ya kuyavamia makanisha mawili katika jimbo la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria.

Nigeria Minna 2025 | watoto waachiliwa huru
Miongoni mwa watoto walioachiliwa baada ya kutekwa na magenge yenye silaha tarehe 22 Disemba 2025 nchini Nigeria.Picha: Chenemi Bamaiyi/AFP/Getty Images

Taarifa zilizotolewa siku ya Jumatatu (Januari 19) zilisema kuwa washambuliaji hao waliyavamia makanisa hayo na kuwalazimisha waumini hao kuondoka nao kuelekea maporini.

Ripoti hizo zilithibitishwa na vyanzo mbalimbali, akiwemo mkuu mmoja wa kanisa, chifu wa kijiji na Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, polisi ya jimbo hilo ilikataa kuthibitisha matukio hayo ilipoombwa na shirika la habari la AFP.

Mashambulizi hayo ya Jumapili ni ya hivi karibuni kabisa katika wimbi la utekaji nyara unaofanywa na magenge yaitwayo majambazi katika taifa hilo la magharibi ya Afrika, ambao huwalenga Wakristo na Waislamu, kwa ajili ya kudai fedha za kikomboleo.

Mnamo mwezi Novemba, magenge hayo yaliwateka zaidi ya wanafunzi na walimu 300 kutoka skuli moja ya Kikatoliki, ambapo 50 walifanikiwa kukimbia na wengine kuachiliwa kwa mikupuo miwili wiki kadhaa baadaye. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW