1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTimor Mashariki

Waumini 600,000 chini Timor Mashariki wasali na Papa Francis

10 Septemba 2024

Takribani waumini laki 600,000 chini Timor Mashariki wanahudhuria misa kubwa inayoendeshwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis.

Papa Francis akiwa Timor ya Mashariki
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akiongoza ibada ya misa akiwa ziarani nchini Timor ya Mashariki, Septemba 10, 2024Picha: Dita Alangkara/AP/dpa/picture alliance

Maelfu ya waumini wamemiminika katika mji mkuu wa Dili ili kumshuhudia Papa Francis mwenye umri wa miaka 87 na kumlaki kwa shangwe alipowasili jana.

Papa Francis alihutubia viongozi wa nchi hiyo, na kupongeza enzi mpya ya amani tangu nchi ilipopata uhuru mwaka 2002.

Aidha kiongozi huyo wa kidini aliwatolea mwito viongozi kukomesha unyanyasaji wa kingono dhidi ya vijana, kashfa ambayo imelikumba Kanisa Katoliki katika miaka ya karibuni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW