1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waumini wa kanisa katoliki wataka mabadiliko ya kisheria DRC

Amina Mjahid
20 Septemba 2019

Waumuini wa kanisa katoliki katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, wametangaza kuanzisha "vita vitakatifu" kupamabana na vitendo vya rushwa nchini humo, huku wakitowa wito wa kujiuzulu majaji 9 wa mahakama ya katiba.

DR Kongo Präsident Kabila einigt sich mit Opposition
Picha: Getty Images/AFP/J. D. Kannah

Kundi hilo la CLC lililokuwa mstari wa mbele kupinga muhula wa tatu kwa rais Joseph Kabila, limeitisha maandamano kote nchini kushinikiza mageuzi kwenye idara ya sheria.

Kamati ya waumini wa katoliki kwa ajili ya mageuzi, CLC imeitisha mandamano juma pili tarehe 1 oktoba kwa sababu mbili. Kwanza ni kuomba kuachishwa kazi kwa maafisa wa serikali waliohusika na kupotea kwa dola milioni 15 zilizotakiwa kuingia kwenye mfuko wa serikali. Pili ni kulazimisha kujiuzulu kwa majaji wote wa koti ya katiba kwa kile wananchoelezea kuwa walihusika na rushwa ya matokeo ya uchaguzi wa rais na bunge.

Kwenye mkutano na wandishi habari, Profesa Isidore Ndaywel, msemaji wa CLC amesema kwamba miezi tisa toka kuitishwa kwa uchaguzi bado hakujafanyika mageuzi waliotarajia na hivyo wanataka mageuzi ya kweli.

"Tunataka kupamba na rushwa, kutotolewa adhabu, na kuwepo na sheria isiyo na nguvu.Kwenye mandamano yetu tutaomba vitu viwili muhimu kwanza kuachishwa kazi kwa watu wote waliohusika na ubadhirifu wa dola milioni 15 za serikali. Pili serikali ichukuwe hatua yakulaazimisha kujiuzulu kwa majaji tisa wa koti ya katiba," alisema Profesa Isidore Ndaywel.

Waumini hao wa kanisa katoliki wamesema wawetoa muda wa wiki mbili ili viongozi wachukuwe hatua muafaka kabla ya manadamano yao.

Rais Tshisekedi aahidi kuchunguza sakata la kupotea kwa mamilioni ya dola 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Felix Felix TshisekediPicha: Presidence RDC/G. Kusema

Rais Felix Tshisekedi alieko ziarani mjini Brussels, Ubeljiji aliahidi kufanya uchunguzi ili kufahamu walohusika na upotevu wa dola milioni 15.

Mwezi juni, serikali ilipoteza? kodi ya dola milioni 15 kwenye baadhi ya makampuni ya mafuta nchini. Kwa mujibu wa mkaguzi mkuu wa taifa ni kwamba fedha hizo hazikuingia kwenye mfuko wa serikali. Huku akitaja baadhi ya watu waliohusika na sakata hilo,mmoja wapo akiwa ni Vital Kamerhe ,kiongozi wa ofisi ya rais.

Kwenye mahojiano na gazeti la  Jeuneafrique, Vital Kamerhe alisema kwamba fedha hizo hazikupotea na siyo yeye anayetakiwa kutoa maelezo ya matumizi ya fedha hizo. Kamerhe ametuhumu baadhi ya watu ambao hakuwataja kwamba wamehusika na kampeni ya kumharibia jina lake.

Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa amesema kwamba uchunguzi umeendeshwa na kuomba kila upande ujizuwiye na taarifa zitakazo vuruga utaratibu wa kisheria. Jambo ambalo CLC wanadai ni kutaka kuwapumbaza wananchi. 

Upinzani kwa upande wake umeomba kueko na uchunguzi huru ilikufahamu ukweli wa sakati hilo la kupotea kwa dola milioni 15.

Chanzo: DW Kinshasa