1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wavuvi ziwa Victoria waomba leseni za A.Mashariki

Musa Naviye13 Oktoba 2022

Wavuvi katika Ziwa Victoria wamehimiza kubuniwa kwa leseni ya pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itakayowezesha wavuvi wa mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania kuendesha shuguli za uvuvi ziwani humo bila vikwazo.

Käfigfischen in Uganda
Picha: DW/Wambi Michael

Wavuvi katika Ziwa Victoria wamehimiza kubuniwa kwa leseni ya pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itakayowezesha wavuvi wa mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania kuendesha shuguli za uvuvi ziwani humo bila vikwazo.

Hatua hiyo inafatia kutokana na wavuvi hao kuendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoongeza ugumu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Gabriel Guda, mwenyekiti wa fuo za majimbo matano yanayopakana na Ziwa Victoria nchini Kenya  Kisumu, Siaya, Busia, Homabay na Migori, anasema sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta zilizotoa ajira kwa kiwango kikubwa katika jumuia hiyo.

Ameongeza kwamba serikali ya Kenya haina budi kwa sasa kufikiria umuhimu  kuangazia maslahi ya wavuvi kadhalika akipendekeza wizara ya Uvuvi kutengwa ili kuwa na ufanisi katika uwajibikaji.

Kuna haja A.Mashariki ibuni leseni kwa wavuvi

Hivi karibuni Rais wa Kenya Willium Ruto alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuna haja ya mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuondoa vikwazo vyote mipakani ili kustawisha usafirishaji na uchumi wa mataifa wanancha.

Mchuuzi wa samaki kutoka kwa wavuvi wanaovua ziwa victoriaPicha: DW/Wambi Michael

Mwenyekiti ufuo wa Homabay Edward Oremo anasema, hatua hiyo inaweza kwenda mbali zaidi ikiwemo kuangalia mipaka ya majini hasa katika ziwa Victoria.

Soma pia:Watu 8 waliozama ziwa Victoria Kenya waendelea kutafutwa

Ameiambia DW kwamba endapo nchi wananchama ambazo ziwa hilo linapatikana hazina budi kuja pamoja na kubuni leseni ambazo zitatolewa kwa wavuvi ili kuendesha shughuli zao bila kadhia ambazo zinashuhudiwa hivi sasa.

Baadhi ya wavuvi ambao wanakubaliana na hoja hiyo wanansema leseni huria itasaidia kukomesha matukio ya wavuvi kutoka Kenya kunyanyaswa na vitengo vya usalama ziwani humo, wakitolea mfano tukio la wavuvi 8 wanaozuiliwa Uganda kwa kushindwa kulipa faini baada ya kutiwa nguvuni mwezi Septemba. 

"Tuanze mfumo huria wa mipaka kwa kuwaruhusu wavuvi ziwani Victoria kuvua, maadamu wanafuata sheria na twawe na leseni" Alisema Gano.

Waziri:Kuangaliwe upya sheria kwa mataifa husika

Waziri wa Uvuvi jimboni Siaya Elizabeth Odhiambo ameunga mkono wazo la rais Ruto la kuwepo mipaka huria sawia na wito wa wavuvi akisema ni hatuaitakayosaidia kuhakikisha sheria zinafanyiwamarekebisho ya pamoja na kusaidia kupambana na ukiukaji wake unapotokea.  Hata hivyo anasema, itamaanisha kuangaliwa upya kwa sheria binafsi za mataifa husika ili kufikia sheria ya pamoja. 

Wavuvi wa samaki ziwa Victoria upande wa UgandaPicha: DW/Wambi Michael

Amesema endapo kutakuwa na mipaka huria ya majini itarahisisha ufuatiliaji kwa maafisa endapo ukiukaji wa sheria utashuhudiwa watakabiliwa licha ya kuwa katika taifa lolote

"Panahitajia mazungumzo, kanuni zinazoshabihiana na maelewano ya pamoja."Alisema waziri Odhiambo.

Katika mazungumzo na mwenzao Joseph Odongo, mwenyekiti wa muungano wa ulinzi wa samaki ziwani Victoria na maziwa mengine madogo nchini Kenya wa Save Fish, anahimiza kufufuliwa kwa sekta ya Uvuvi Ziwani Victoria na kuangaziwa kwa changamoto zinazoandamana na sekta hiyo ikiwemo usimamizi, uendeshaji huduma na uvuvi haramu.

Soma pia:Watu watano wamekufa baada ya mashua yao kuzama Ziwa Victoria

Katika ziara yake nchini Uganda akihudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa taifa hilo, rais Ruto wa Kenya alitoa wito kwa marais wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kuondoa vikwazo vya mipaka anavyosema vinachangia mkwamo wa biashara huria katika ukanda huu.

Katika maahimisho hayo, rais wa Uganda Yoweri Musevenialisema maendeleo katika Jumuiya hii yatafanikiwa zaidi endapo raia wa mataifa yote wataruhusiwa kusafiri na kuendesha biashara bila vikwazo.

Uvuvi wa aina yake Nakuru

03:23

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW