Wawili wafa kwenye uvunjwaji wa madrasa India
9 Februari 2024Maafisa wa manispaa katika jimbo la kaskazini la Uttarakhand walivunja majengo ya madrasa siku ya Alkhamis (Februari 8) wakidai kwamba yalijengwa bila kibali.
Polisi imesema waandamanaji Waislamu waliwarushia mawe wakati wa maandamano yaliofuatia uvunjaji huo, na wakajibu kwa kufyatua gesi ya kutoa machozi.
Soma zaidi: Wahindu washambuliana na Wakristo India
Mamlaka katika mji wa Halswani ilisitisha huduma za intaneti, kufunga shule, kutangaza marufuku ya kutembea nje na kupiga marufuku mikusanyiko mikubwa baada ya kuzuka vurugu hizo.
Makundi ya siasa kali ya Wahindu yamepata nguvu katika kampeni yao dhidi ya majengo ya Waislamu tangu Waziri Mkuu Narendra Modi alipoingia madarakani muongo mmoja uliopita.
Mwezi uliopita, Modi alizindua hekalu jipya la Kihindu katika mji wa kaskazini wa Ayódhya, lililojengwa kwenye eneo la msikiti wa karne kadhaa, ulioharibiwa na wanazi wa Kihindu mwaka 1992.