Wawili wafariki baada ya maandaano Arusha
6 Januari 2011Maandamano hayo yalioyandaliwa na viongozi wa chama cha upinzani cha CHADEMA yalifanyika hapo jana na wengine 9 wamejeruhiwa wakiwemo maafisa wa polisi.Akizungumza na waandishi wa habari,mkuu wa polisi wa eneo la Arusha,Tobias Andengenye,alizithibitisha taarifa hizo na kwamba wawili hao walifariki wakiwa hospitalini na wengine 49 wanazuiliwa na polisi .Maelfu ya wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA walikusanyika mjini Arusha ili kuupinga ushindi wa Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka uliopita.
Kwa sasa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi wakiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chama,Dr Wilbrod Slaa.
Itakumbukwa kuwa Dr Wilbrod Slaa aliwania uchaguzi huo na kuibuka wa pili kwenye kinyang'anyiro hicho.Kadhalika Dr Slaa alikuwa mstari wa mbele kuifichua kashfa ya ufisadi iliyomfanya Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kujiuzulu kufuatia tuhuma pamoja na wabunge na gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.Kulingana na polisi wafuasi hao wa CHADEMA walipaswa kufanya mkutano na wala sio maandamano.Hii leo polisi wa kupambana na ghasia wanaripotiwa kupiga doria mjini Arusha kuliko na makao ya mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda,ICTR.
Mwandishi:Mwadzaya,Thelma/RTRE-AFPE Mhariri:Charo,Josephat