1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUhispania

Wazee 10 wafariki Uhispania katika ajali ya moto

15 Novemba 2024

Watu 10 wamekufa kufuatia ajali ya moto iliyotokea mapema leo kwenye nyumba wanakoishi wastaafu katika mji wa kaskazini mwa Uhispania wa Villafranca del Ebro.

Moja ya mikasa ya moto Uhispania
Mikasa ya moto imekuwa ikiikumba Uhispania mara kwa mara. Picha: Alberto Saiz/AP/picture alliance

Watu wawili wamo katika hali mbaya baada ya kuvuta hewa yenye sumu.

Fernando Beltran, afisa mkuu wa serikali ya kitaifa katika eneo hilo, amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi na moja alfajiri na wahanga ni wazee waliokuwa wakiishi katika nyumba hiyo iliyofahamika kwa jina la "Jardines de Villafranca".

Vikosi vya zima moto kutoka mji ulio jirani wa Zaragoza ulio umbali wa kilometa 35, vilihitaji karibu masaa mawili ili kuudhibiti moto huo ambao chanzo chake bado kinachunguzwa.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW