1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Wazima moto Uturuki wadhibiti moto katika mikoa miwili

16 Agosti 2024

Wazimamoto nchini Uturuki wamefanikiwa kuudhibiti moto katika mkoa mmoja kati ya minne kulikozuka moto mkubwa wa nyika.

Türkei | Waldbrände nahe Kumkoy auf der Halbinsel Gallipoli
Picha: Sercan Ozkurnazli/AP Photo/picture alliance

Waziri wa kilimo na misitu Ibrahim Yumakli amesema leo kuwa, juhudi zinaendelea kudhibiti moto katika mikoa iliyobakia.

Moto mkubwa ulizuka kaskazini magharibi mwa Uturuki mapema wiki hii katika mikoa ya Canakkale, Bolu, Manisa na Gordes.

Waziri huyo ameeleza kuwa, moto uliozuka katika mkoa wa Canakkale umedhibitiwa huku wazima moto wakifanikiwa kudhibiti japo kwa kiasi fulani moto katika mkoa mwengine wa Manisa.

Magavana wa Canakkale na Bolu wamesema watu katika baadhi ya vijiji wamehamishwa kama hatua ya tahadhari lakini hakuna tishio la moja kwa moja kwa maeneo ya makaazi ya watu.