Wazir Mkuu Brown akataa kukaa meza moja na Rais Mugabe
28 Novemba 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema hatohudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Bara Afrika utakaofanywa Desemba 8 na 9 nchini Lisbon.Brown ameamua kutoshiriki kwenye mkutano huo,baada ya Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe kusema kuwa atahudhuria mazungumzo hayo.Brown amesema,hayupo tayari kukaa meza moja na Mugabe anaetawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1980 na akishutumiwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Ureno,ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka,imekosolewa kwa kumualika Rais Mugabe.Lakini viongozi wa Kiafrika wamesema hawatohudhuria mkutano huo ikiwa Mugabe atapigwa marufuku.