1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri ajiuzulu kwa kukiuka vizuizi vya COVID

31 Januari 2022

Waziri wa mambo ya ndani wa Hong Kong amejiuzulu baada ya kuhudhuria sherehe pamoja na maafisa wenzake na kukiuka sheria ya kujizuia na mikusanyiko ya watu wengi ili kukabiliana na mlipuko wa maambukizi ya COVID-19

China Hongkong | Carrie Lam und Caspar Tsui Ying-wai
Picha: Nora Tam Photo via Newscom/picture alliance

Waziri wa mambo ya ndani wa Hong Kong Caspar Tsui amejiuzulu leo Jumatatu, wiki kadhaa baada ya kuhudhuria sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwakilishi wa Hong Kong kwenye bunge la kitaifa la China.

Sherehe hiyo haikuwa halali kwa wakati huo, kwa kuwa mkuu wa kitengo cha afya cha jiji tayari alikuwa ameonya watu kujiepusha na mikusanyiko mikubwa baada ya mlipuko huo.

Pamoja naye, alikuwepo mwanachama wa chama cha tawala cha People's Congress Witman Hun. Lakini pia kulikuwa na zaidi ya watu 200, ikiwa ni pamoja na maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la polisi la Hong Kong na uhamiaji pamoja na wakuu wa taasisi ya kupambana na ufisadi. Wabunge takribani 20 pia walikuwepo.

Soma Zaidi: Boris Johnson: Shujaa wa Brexit chini ya shinikizo la 'partygate' 

Orodha hiyo ya wageni waliohudhuria ilifichuliwa baada ya mamlaka za afya kumfuatilia mtu mmoja aliyeambukizwa ambaye pia alihudhuria sherehe hiyo. Tukio hili limekuwa aibu kubwa kwa kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam ambaye serikali yake inatekeleza sera ya "ziro-COVID", inayofanana na ya Beijing.

Mamlaka zimesema Tsui hakutumia App ya kufuatilia wakati alipoingia kwenye mgahawa kulikofanyika sherehe hiyo, ambayo ni lazima kuizumia kwa sasa. Lakini pia hakuvaa barakoa, licha ya masharti yaliyo wazi kwamba wanatakiwa kuvaa wakati wote.

Uingereza inataraji kupitia upya sera yake ya kuchanja kwa lazima kwa watumishi wa umma kabla ya mjadala wa bunge.Picha: PRU/AFP

Uingereza kupitia upya sera ya chanjo ya lazima

Uingereza: Taifa hilo linaangazia kuupitia tena uamuzi wake wa kuifanya chanjo ya COVID-19 kuwa ya lazima kwa watumishi wa afya nchini humo, wakati kukiwa na wasiwasi kwamba sekta hiyo huenda ikapoteza watumishi maelfu ya watumishi wake.

Sera ya watumishi hao kuwa wamechanjwa wote ifikapo Aprili 1, ilitangazwa Novemba 2021. Hata hivyo ilipata ukosoaji mkali kutoka kwa baadhi ya watumishi waliotoa maonyo kwamba kuwafukuza waliogoma kuchanja kutachangia upungufu mkubwa wa watumishi. Wabunge wa chama cha kihafidhina cha waziri mkuu Boris Johnson pia waliikosoa sera hiyo.

Gazeti la Daily Telegraph limeandika mapema leo kwamba sera ya ulazima wa chanjo inaweza kuondolewa, wakati kukitarajiwa taarida zaidi kutoka kwa waziri wa afya, Sajid Javid baadae leo.

Ujerumani bado inajikongoja kufikia lengo la chanjo.

Ujereumani bado haijafikia lengo lake la kuchanja watu wake kwa asilimia 80 kama ilivyokusudiaPicha: Robin Utrecht/picture alliance

Ujerumani: Serikali imeshindwa kufikia lengo lake la kuwachanja asilimia 80 ya watu wake kabla ya kufikia mwishoni mwa mwezi huu, ikiwa ni kama mwezi mmoja hivi kabla wabunge kupigia kura muswada wa sheria ya kuifanya chanjo kuwa ya lazima.

Afrika na Mashariki ya Kati: Wizara ya afya ya Qatar imesema jana Jumapili kwamba imeidhinisha chanjo ya Pfizer-BioNTech kwa watoto wa kati ya miaka 5-11. Mwezi Novemba, mataifa ya Ghuba Bahrain na Saudi Arabia yaliidhinisha chanjo ya Pfizer kwa matumizi ya dharura kwa watoto wa miaka kama hiyo.

Na huko Algeria, kumeripotiwa kisa cha kwanza cha kirusi cha Omicron cha BA.2, hii ikiwa ni kulingana na kituo cha televisheni cha Ennahar kilichomnukuu mkurugnezi mkuu wa taasisi ya Pasteur jana Jumapili.

Taifa hilo la Afrika Magharibi limerekodi visa vipya 1,742 vya COVID-19 na vifo 10, na kufanya jumla ya visa kufikia 249,310 na vifo 6,555, hii ikiwa ni kulingana na takwimu rasmi.

Mashirika: RTRE/DW

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW