Waziri Berlin ashtakiwa kwa hali mbaya ya wakimbizi
11 Desemba 2015Mazingira nje ya ofisi ya afya na ustawi wa jamii LaGeSo mjini Berlin yemegeuka fedheha ya kitaifa kwa Ujerumani. Kila siku mamia ya wakimbizi hurundikana kwenye vizuwizi vya chuma nje ya ofisi hiyo ya wizara ya afya na ustawi wa jamii ya jimbo, ambayo uwa wake uligeuka eneo la kusubiria wakati fulani majira ya joto. Watu hao wanaelekeza usikivu wao kwenye ubao mweusi wa kielekttroniki unaoonyesha namba za njano - na mara nyingi kunakuwepo na mgandamizo na ongezeko la watu kila wakati namba mpya inapojitokeza.
Matukio katika ofisi ya LaGeSo hayajatoa chochote zaidi ya habari mbaya kwa mji mkuu huo wa Ujerumani. Nafasi ya taarifa za habari za awali, kuhusu watu kusubiri kwa siku na wiki kuasajiliwa, ilichukuliwa mwezi Oktoba, na ripoti na mashambulizi ya kimwili na nyimbo za wanazi mamboleo zilizokuwa zinaimbwa na walinzi waliokodiwa na serikali ya Berlin kulinda usalama. Kampuni iliyokuwa imepewa kazi hiyo iliondolewa tangu wakati huo na nafasi yake kupewa kamouni nyingine.
Kumekuwepo pia na ripoti za majeruhi na kuuguwa kwa wakimbizi - Novemba 14 wafanyakazi wa kujitolea walilazimika kuita gari la kubebea wagonjwa baada ya mwanaume aliekuwa anasubiri kwenye foreni kuonnyesha dalili za kuishiwa maji mwilini, ambapo muhudumu wa dharura alimpima baadae na kugundua kuwa joto lake la mwili lilikuwa limefikia kiiwango cha nyuzi 32 za celsius.
Serikali yatakiwa kutoa maelezo
Sasa kundi la mawakili 40 wamefungua mashtaka ya kusababisha majeraha ya kimwili dhidi ya waziri wa afya na ustawi wa kijamii Mario Czaja na mkuu wa ofisi ya LaGeSo Franz Allert, kwa kuruhusu hali hiyo kuendelea. "Mazingira kama ya Berlin ni ya kipekee nchini kote," alisema wakili Christina Clemma katika taarifa iliyochapishwa siku ya Jumatatu na Umoja wa mawakili wa Kidemokorasia (VDJ), ambalo ni moja ya mashirika yaliyofungua mashtaka hayo. "Hakuna jimbo lolote longine la Ujerumani walikofeli wanasiasa na utawala kama ilivyo hapa."
"Tuna taarifa za mwanamke mjamzito aliezimia, za majeraha yaliyosababishwa na mkanyagano kwa mfano," wakili Ulrich von Klinggraeff aliiambia DW. Tumeanda orodha ndefu, lakini tumechukuwa ripoti kutoka kwa shirika la kujitolea la 'Moabit Hilft' na kuchukuwa baadhi ya kesi za sampuli."
Tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo, von Klinggraeff amepokea barua pepe kutoka kwa watu wanaojitolea kutoa taarifa zaidi. "Mwalimu anaetoa masomo ya Kijerumani kwa wakimbizi alinieleza kuhusu mmvulana mkimbizi aliechoka kabisaa ambaye alianguka darasani kwake," alisema. "Alimuambia kwamba alikuwa amepanga foreni kwenye ofisi ya LaGeSo tangu saa 10 alfajiri, na alimuonyesha jeraha bichi kwenye mkono wake ambalo alisababishiwa na moja kati ya walinzi.
Katika mashtaka hayo, mawakili wametoa orodha ya mashahidi wakiwemo wafanyakazi wa kujitolea, waandishi habari, wafanyakazi w amashirika yasiyo ya kiserikali na vile vile Dk. Guenther Jonitz, rais wa chama cha madaktari wa Berlin, ambaye amekosoa waziwazi mazingira ya LaGeSo.
Berlin ya kipekee
Lakini von Klinggraeff anakiri kuwa hakuna uwezekano mkubwa kwa waendesha mashtaka wa jimbo kumfungulia mashtaka Czaja - Ni nadra kwa wanasiasa waliochaguliwa kushtakiwa kwa kushindwa kwa mamlaka wanazoziongoza. "Bila shaka nina matumaini kuwa waendesha mashtaka wataona haja yakufanya hivyo," alisema. "Lakini wakati huo huo, zingatio tulilolipata kutoka kwa vyombo vya habari tangu jana ni mafanikio tayari. Na natumani kuwa shinikizo la kijamii dhidi ya bwana Czaja litazaa matunda."
Ni kweli kwamba Berlin ni moja ya tawala masikini zaidi za umma nchini Ujerumani wakati mwingi, lakini hiyo siyo sababu kwa mujibu wa Klinggraeff: " Kukosa rasilimali katika mji kama Berlin ni jambo la ajabu," alisema. "Hilo ni suala linalohusiana na vipaumbele vya kisiasa. Unapata hisia kwamba mazingira ya huko ni mabaya sanakwa sababu watu wanachukuliwa kama raia wa daraja la pili. Inaweza kuwa tu kwamba kwa serikali ya Berlin, au kwa bwana Czaja, udhibiti na utulivu vinatangulizwa kabla ya haki ya watu kuwa salama kimwili."
Majibu ya Czaja kuhusu kesi hiyo yalikuwa ya kimadharau. "Kila moja yuko huru kufungua mashtaka, lakini hilo halitosaidia kuboresha hali ya wakimbizi," waziri huyo aliviambia vyombo vya habari vya ndani. "Tuhuma kwamba utawala ulichochea majeraha na ugonjwa kwa maksudi zinasikitisha. Nalipinga hilo kabisaa. Tunafanya kazi kila siku kuzuwia ukosefu wa makaazi."
Vurugu ndani na nje
Berlin imekuwa ikipambana kushughulikia kile ambacho kinakadiriwa kuwa wakimbizi 800 wanaowasili kila siku. Licha ya kuwa na wafanyakazi wa dharurua na hata wanajeshi kuchukuwa majukumu ya kiutawala, vurugu zinazoshuhudiwa nje ya LaGeSo zinaonekana kuakisiwa hata ndani.
Kituo cha utanganzaji cha mji huo RBB kilikusanya ripoti kadhaa za kutisha kutoka kwa maafisa ambao hakikuwataja majina kutoka ofisi hiyo. "Maombi yasiyoshughulikiwa yemejazana kwenye kwenye maboksi ya barua ya njano," afisa mmoja alisema. "Na maboksi ya njama yanahifadhiwa katika vyumba kadhaa. Hakuna mfumo wa kuagiza ndiyo maana tuna kazi ya 'mtafutaji' - hao ni wenzetu wanaojishughulisha tu na kazi ya kutafuta mafaili sahihi."
Tunawaita wakimbizi 500 au zaidi kila siku - wakiwa na miadi ya saa tatu asubuhi," alisema mwingine. "Lakini tumejua kwa wiki kadhaa kwamba tunaweza kushughulikia watu 200 sanasana. Kila nawauliza wakubw azangu kwa nini tusitoe miadi inayotimizika. Jibu ninalopata ni kwamba pengine inahusu maagizo fulani au nyingine kwamba laazima tufuate tunachoambiwa."
Mwandishi: Benjamin Knight/DW
Tafisri: Iddi Ssessanga
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman