1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri Blinken aunga mkono mahusiano ya China-Korea Kusini

17 Juni 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Anthony Blinken amesema anaunga mkono juhudi za Korea Kusini za kuimarisha zaidi ushirikiano imara baina yao na China

USA, Washington | Antony Blinken
Picha: Mandel Ngan/Pool/AP/picture alliance

Blinken, aliyewasili Beijing tayari kwa ziara ya afisa wa ngazi za juu zaidi wa serikali ya Joe Biden kufanywa nchini humo, alizungumza kwa simu na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Park Jin, na kujadiliana juu ya mahusiano baina ya mataifa hayo, uhusiano kati ya Korea Kusini na China pamoja na Korea Kaskazini.

Hata hivyo, maafisa wa Marekani wameonyesha matumaini hafifu juu ya ziara hiyo ya Blinken nchini China ambayo ni ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano, ikiwa itafungua njia ya namna Washington na Beijing zitakavyoshughulikia masuala baina yao.

Kulingana na Blinken, ziara hiyo inalenga kuanzisha mawasiliano ya wazi na thabiti baina yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW