1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Waziri Gabby Bugaga apatikana amekufa Burundi

16 Aprili 2026

Maiti ya waziri wa Burundi anayehusika na utangazaji habari na ufundi wa kisasa wa mawasiliano Gabby Bugaga imepatikana asubuhi hii katika eneo la Tabarare la kivoga umbali wa kilometa 20 kaskazini mwa Bujumbura.

Burundi Gefängnis Feuer Brand Gitega
Picha: ASSOCIATED PRESS/AP/picture alliance

Kwa muda mfupi wa majukumu yake ya uwaziri, Gabby alionekana kufuatilia kwa karibu uandishi habari na kuboresha kazi za mitandao ya kijamii husuan Yuotube. Ni hayati Gabby Bugaga katika mahojiano na DW muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa habari na ufundi wa kisasa wa mawasiliano.

Mwili wake waziri Gabby Bugaga umeonekana ndani ya gari lake la kiwaziri asubuhi ya leo katika eneo la tabarare la Kivoga umbali wa kilometa 20 kaskazimi mwa Bujumbura, eneo kunakolimwa vigasi.

Gari lake hilo limeonekana kuharibika sehemu ya nyuma na sehemu ndogo ya upande wa kushoto kuliko na usukani huku mwili wake waziri ukiwa umeinamia sehemu ya kulia. Hata hivyo hakujaonekana gari alilogongana nalo ama kilichosababisha ajali hiyo. Hali iliyozusha duku duku juu ya sababu za kifo chake.

Kifo cha Bugaga chaacha simanzi kubwa Burundi

Ni kwenye majira ya saa 2 unusu ndipo timu ya mawaziri yule wa mambo ya ndani na usalama, waziri wa sheria pamoja na katibu mkuu aliye pia msemaji wa serikali walipowasili eneo la tukio na hatimaye maiti yake Gabby Bugaga kuondolea.

Kifo chake Gabby Bugaga waziri wa habari Burundi kimeacha simanzi kubwa katika ulimwengu wa waandishi habari nchini ambapo kwa muda mfupi amekalia kiti cha uwaziri Gabby Bugaga alionekeana kuboresha mengi katika sekta hiyo.

Mousses Habyarimana aliyefanya naye kazi kwenye kituo cha Redio na Televisheni ya taifa, anasema Gabby ameliacha pengo kubwa kwani alikuwa akiitambuwa kazi ya uandishi na kujaribu kuiboresha.

Kwa upande wake Haidallah Hakizimana muandishi pia wa habari anasema waziri Gabby Bugaga ameliacha pengo ambalo itakuwa vigumu kuliziba.

Hadi wakati huu nikiripoti bado hakujatolewa tamko rasmi la serikali kuhusiana na kifo cha waziri wake wa habari na ufundi wa kisasa wa mawasiliano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW