Waziri Gerd Mueller kufanya ziara barani Afrika
21 Agosti 2018Biashara huria ama biashara bila kutoza ushuru kwa muda mrefu sio tena mada muhimu, kwasababu kwa muda mrefu bidhaa kutoka Afrika zimeingia katika mataifa mengi ya bara la Ulaya, amesema mtaalamu wa maendeleo ya kiuchumi Robert Kappel katika mahojiano na DW. Mara nyingi mada kuhusu ruzuku katika mazao pamoja na vizuwizi vya biashara yamekuwa masuala yanayozungumzwa sana. Profesa kutoka chuo kikuu cha Leipzig anaishutumu Ulaya kwa ukoloni mamboleo katika sera za fedha. Mada hii lakini anaiweka kando waziri Mueller , hususan wakati huu wa ziara yake katika bara la Afrika. Anashindwa kuelewa kwamba yeye ndie amepanua mwanya wa kutokuwa na usawa katika biashara na kuwa mkubwa zaidi katika miaka iliyopita, licha ya kuwapo uhuru wa kutokuwa na ushuru.
Kappels amedokeza kwamba waziri hana taarifa sahihi na anapaswa kukosolewa. Uhusiano wa kibiashara baina ya Ulaya na Afrika unazidi kukua kinyume na manufaa ya Afrika. Wakati katika baadhi ya nchi za Afrika bidhaa zinazoingizwa kutoka Ulaya na hususan Ujerumani zinaongezeka kidogo, mauzo ya bidhaa kutoka Afrika kwenda Ulaya katika baadhi ya nchi za Afrka idadi inapungua.
Hii inatokana hususan katika suala la bei, anasema Robert Kappel. Kutoka Afrika bidhaa inayoingia katika mataifa ya Ulaya inakuwa ni mafuta na gesi ya ardhini kuja Ujerumani na mataifa ya Ulaya zikifuatiwa na mazao ya shambani. Bei ya mazao ya shambani na pia mafuta na gesi katika miaka ya hivi karibuni zimepungua. Na ndio sababu uwiano wa kibiashara kati ya nchi za Afrika na Ulaya umeingia katika hali ya kutowiana."
Udanganyifu wa kibiashara
Kwa mujibu wa tarakimu za shirika la mahitaji ya kibiashara la Ujerumani la Germany Trade and Invest kulikuwa na udanganyifu wa biashara ya nje ya Ujerumani pamoja na mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara unaofikia euro bilioni 26 katika miaka iliyopita. Kwa sababu Afrika kusini mwa jangwa la Sahara katika mwaka 2017 kwa biashara ya asilimia 1.1 tu ilipoteza sehemu ndogo ya biashara jumla kama ilivyokuwa katika mwaka mmoja uliopita.
Kwa dhamira ya Umoja wa Ulaya na pia serikali ya Ujerumani, hapo baadaye bidhaa nyingi zaidi za Ulaya zitaingia katika soko la Afrika. Kwasababu katika wakati huo mataifa ya ulaya yamegundua kwamba Afrika ni soko muhimu. Hadi ifikapo mwaka 2050 robo ya wakaazi wa dunia watakuwa wanaishi katika bara la Afrika , inaeleza taasisi ya takwimu ya Ulaya, Eurostat. Afrika itakuwa dude kubwa lililolala katika uchumi wa dunia", wanasema mjini Berlin na Brussels. Na soko hili muhimu hawataki kuliacha bila mapambano kwa mikononi mwa Wachina na Wahindi. Biashara na mataifa ya Asia na Afrika inaongezeka kwa miaka kadhaa sasa na ina umuhimu mkubwa katika ukubwa wake.
Tangu muda mrefu Umoja wa Ulaya umekuwa ukifanya majadiliano na nchi za Afrika kuhusiana na mkataba mpya wa kibiashara, unaofahamika kama makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi EPA. mkataba huo unataka kufunguliwa kwa ukamilifu masoko kwa ajili ya bidhaa za Ulaya katika soko la Afrika. Waungaji mkono wanamatumaini kupata soko muhimu kwa pande zote mbili, na kuongeza ufanisi kupitia ushindani, na bei za chini kwa watumiaji.
Katika ziara yake ya wiki moja waziri Mueller kuanzia siku ya Alhamis atafanya ziara katika nchi saba za Afrika. Baada ya Eritrea, Ethiopia, Msumbiji, Botswana, Zimbabwe na Chad , atamalizia ziara yake nchini Ghana. Katika mazungumzo yake na kansela wa Ujerumani na rais wa Ghana Nana Akufo-Addo kutakuwa na suala la mabadiliko ya ushirikiano kwa nchi hizo mbili pamoja na uwezekano wa uwekezaji.
Mwandishi: Cascais, Antonio / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman