1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Clinton kutembelea nchi saba barani Afrika.

Abdu Said Mtullya28 Julai 2009

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ataanza ziara ya nchi saba barani Afrika wiki ijayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton anatarajiwa kuzitembelea nchi za Afrika wiki ijayo.Picha: AP

WASHINGTON:

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton anapanga kukutana na rais wa serikali ya mpito ya Somalia Sheikh Sharif Ahmed.Waziri Clinton atakutana na rais huyo wakati wa ziara yake ya nchi saba barani Afrika itakayoanza wiki ijayo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imearifu kuwa waziri Clinton atakutana na kiongozi huyo wa Somalia mjini Nairobi wakati atakapohudhuria kikao cha mwaka cha masuala ya biashara baina ya Marekani na nchi za Afrika.


Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW