1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Bangladesh yamuapisha waziri mkuu wake mpya

17 Februari 2026

Tarique Rahman anakuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamme nchini Bangladesh tangu mwaka 1991

Waziri mkuu mpya wa Bangladesh Tarique Rahman
Waziri mkuu mpya wa Bangladesh Tarique RahmanPicha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Waziri mkuu mpya wa Bangladesh Tarique Rahman ameapishwa madarakani leo baada ya chama chake kupata ushindi wa kishindo kufuatia uchaguzi wa bunge uliofanyika wiki iliyopita.

Uchaguzi huo ni wa kwanza tangu liliposhuhudiwa vuguvugu la maandamano makubwa mwaka 2024 yaliyomuondowa madarakani Sheikh Hasina.

Tarique Rahman wa BNP aongoza matokeo ya awali Bangladesh

Tarique Rahman atakayeiongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo pia ni waziri mkuu wa kwanza mwanamme nchini Bangladesh katika kipindi cha miaka 35.

Tangu mwaka 1991 nchi hiyo imekuwa ikitawaliwa na mawaziri wakuu wanawake.

Mawaziri kadhaa pamoja na viongozi wengine katika serikali mpya pia wameapishwa hivi leo katika shughuli iliyoongozwa na rais asiyekuwa na mamlaka makubwa, Mohammed Shahabuddin.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW