1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu mpya wa Haiti aahidi kutafuta umoja wa kitaifa

30 Mei 2024

Waziri Mkuu mpya wa Haiti Garry Conille ameahidi kutafuta umoja wa kitaifa katika ujumbe wake wa kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo na Baraza Tawala la nchi hiyo inayozongwa na uhalifu wa magenge ya wahuni.

Polisi wa Haiti wakiwa kwenye doria dhidi ya magenge ya uhalifu
Polisi wa Haiti wakiwa kwenye doria dhidi ya magenge ya uhalifuPicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Kwenye ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Conille ayeliwahi hapo kabla pia kuwa waziri mkuu wa Haiti kati ya Oktoba 2011 hadi Mei 2012 amesema ananuwia kufanya kazi pamoja na makundi yote nchini humo kufanikisha hatma njema kwa watoto wa taifa hilo.

Soma pia:Biden na Ruto kukutana mjini Washington

Ametumia ujumbe huo pia kuwashukuru makundi ya kiraia, vyama vya siasa na raia wa Haiti waishio nje ya nchi kwa kulipendekeza jina lake ili ateuliwe kuchukua nafasi ya waziri mkuu.


Kazi kubwa inayomkabili ni kupambana na uhalifu wa magenge ambayo yanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu, Port au Prince na kurejesha utulivu na amani nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW