1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu mpya wa haiti Conille aapishwa

4 Juni 2024

Garry Conille ameapishwa kama Waziri Mkuu mpya wa Haiti hapo jana. Conille ameahidi kuleta suluhu la matatizo yanayolikumba taifa hilo la Caribbean ambalo kwa sasa linakabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama.

Haiti | Garry Conille pamoja na Edgard Leblanc Fils
Rais wa Baraza la Urais wa Mpito wa Haiti Edgard Leblanc Fils Kushoto akizungumza na Waziri Mkuu wa Haiti, Garry Conille Kulia.Picha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Conille aliteuliwa na baraza la mpito la rais lililokuwa linaiendesha nchi hiyo kufuatia kuachia ngazi mnamo Aprili kwa Waziri Mkuu Ariel Henry, wakati ambapo machafuko yanayotokana na magenge yalipoongezeka.

Kuapishwa kwake sasa kunampa mamlaka ya kuunda serikali kwa kushauriana na baraza hilo.

Conille aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa haiti kwa kipindi kifupi kati ya mwaka 2011 hadi 2012.

Soma pia:Waziri Mkuu mpya wa Haiti aahidi kutafuta umoja wa kitaifa

Machafuko yanayosababishwa na magenge yameizonga nchi hiyo na mwishoni mwa mwezi Februari makundi yaliyojihami yalifanya mashambulizi katika maeneo kadhaa ya kimkakati katika Mji Mkuu Port-au-Prince yakidai kwamba yanataka kumpindua Waziri Mkuu Henry. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW